Tanzanian forum: Other - MATATIZO SUGU BARANI AFRICA
Share this topic
7 Mar 2016 14:52

Ndugu zangu wa Tanzania na wabara zima la Africa, lengo na madhumuni ya kuwaletea mada hii ni masikitiko na masuto yatokayo ndani ya moyo wangu kulihusu bara letu zuri la Africa., Baa la njaa, latizo la maji, uongozi mbaya kutoka kwa viongozi wetu, udikteta, ukabila, ugaidi, kufuturu kwa migogoro kwa bahadhi ya nchi kama Congo DR, somalia, Sudan hususan eneo la Darfur, jamuhuri ya Africa ya kati nk, hayo nibaadhi ya matatizo sugu yanayo likumba bara letu zima la Africa pamoja na sisi kama Waafrika., kwanini iko hali hii ndugu zangu waafrica???, Je mwadani ninini chimbuko la yote haya??? na ninini suluhisho la kudumu la hayo yote???. Kufikia hapo nawaombeni ushirikiano wenu katika kulichambua suala hili zito na muhimu kwetu, Ahsanteni

Edited by KERO ALI / 8 Mar 2016 18:15
1 Apr 2016 21:19

m nahisi yote haya yanalewa na mfumo wa kuto aminiana na kuto aminika hivo mpasuko au mwingiliano wa mawazo tofauti tofauti ndo huleta mpasuko wa mawazo na hujenga kila mtu aamin anacho amin kua ni sahih kulko mwngine hivo migogoro huanzia apo

Edited by zedon77 / 2 Apr 2016 08:34
26 Jun 2016 17:53

Hii ilitokana na wakoni kuchukua maliasili za afrika na nguvu kazi. nakupeleka kwao. pia uongozi mbaya na usimamizi.

30 Jun 2016 08:36

Uroho wa madaraka na tamaa za kushawishiwa na mataifa makubwa ndio mzizi wa kuzalisha fujo, vita ya wenyewe kwa wenyewe.

28 Jul 2016 08:38

kwa upande wangu nahis ubinafsi ndo unaofanya yatokee haya yote..

26 Feb 2017 12:10

axant xan mungu akubrk.

7 May 2017 09:39

Tatizo kubwa ni UBINAFSI na kutokuwa na roho ya huruma kwa viongozi wa kiafrika.